Monday, September 9, 2013

GRADUATION YA T.Y.C.S LYUSA SEKONDARI.

GRADUATION YA T.Y.C.S ILIYOFANYIKA TAREHE  07/09/2013,

TUTAKUKUMBUKA MWALIMU THOBIAS YANAS MNZAVA.

MWALIMU THOBIAS YONAS MNZAVA ALIFARIKI TAREHE 16/08/2013 KATIKA WILAYA YA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA KWA AJARI YA PIKIPIKI.MWALIMU THOBIAS MNZAVA KATIKA UHAI WAKE ALIAJIRIWA TAREHE 01/02/2012 KAMA MWALIMU WA SEKONDARI DARAJA LA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI LYUSA.AKIFUNDISHA MASOMO YA HISTORY NA GEOGRAPHY VILEVILE ALIKUA MWALIMU WA AFYA."WE WILL MISS YOU THOBY" MUNGU AMETOA MUNGU AMETWA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.AMEN

Saturday, May 18, 2013

MITIHANI YA MUHULA WA KWANZA 2013 LYUSA SEKONDARI.


PICHANI JUU WANAFUNZI WA LYUSA SEKONDARI KIDATO CHA PILI WAKIWA KATIKA MITIHANI YA KUMALIZA MUHULA WA KWANZA ILIYOANZA TAREHE 13/05/2013 NA KUMALIZIKA TAR 20/05/2013PICHANI CHINI NI WANAFUNZI WA  KIDATO CHA NNE WAKIJIANDAA KUINGIA KATIKA MTIHANI WA KANDA ILIYOANZA TAR 13/05/2013.

DIWANI ATEMBELEA MAENDELEO YA UJENZI WA MAHABARA.



DIWANI WA KATA YA NKOMA WILAYA YA MEATU BWANA ELIA GANDE KUTOKA KULIA AKIAMBATANA NA MWALIMU MKUU WA LYUSA SEKONDARI MWL DEOGRATIUS MAGESA KUTOKA KUSHOTO.WAKIWA KATIKA UKAGUZI WA MAENDELEO YA JENGO LA MAHABARA SHULENI HAPO NA KUSIFU KASI YA UJENZI YA INAYOENDELEA SHULENI HAPO.

Saturday, April 27, 2013

LYUSA WATEMBELEA KIMALI

Timu za mpira wa miguu (Wasichana) Kimali na Lyusa zikiwa katika mpambano mkali  na wakusisimua.

Timu ya shule ya sekondari Kimali katika picha ya pamoja.

 Timu ya shule ya sekondari Lyusa katika picha ya pamoja.

UJIRANI MWEMA

Timu za mpira wa miguu (Kimali na Lyusa Shule ya Sekondari) zikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mpambano ambao hadi unaisha timu ya Kimali ilikuwa ikiongoza.

 
Timu ya shule ya sekondari Kimali katika picha ya pamoja.



Timu ya shule ya sekondari Lyusa katika picha ya pamoja.

Sunday, April 21, 2013

ADHA YA MVUA!!!

Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekwama baada ya mto kufurika maji.

Hivi ndiyo mauzurio ya wanafunzi yanavyokuwa wakati wa msimu wa mvua.





UJENZI WA MAABARA YA SAYANSI (updated)


Hatimaye baada ya miaka mitano (2008-2013)  kupita ujenzi wa maabara ya sayansi umeanza kwa kasi ya ajabu. Pichani ni mafundi wakiendelea na kazi yakujenga maabara hiyo.
Mafundi wakiendelea na kazi yakujenga maabara.

 Mafundi wakiendelea na kazi yakujenga maabara.

Thursday, March 14, 2013

UMISETA MEATU.

TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA WASICHANA  KIMALI SEC  IKIJIANDAA KUCHEZA NA TIMU YA MEATU SEC.
TIMU YA MPIRA WA PETE YA LYUSA SEC.
WANAFUNZI WAKIELEKEZWA KUKIMBIA RIADHA SIKU YA UMISETA.

WANARIADHA KUTOKA SHULE MBALIMBALI WAKIJIANDAA KWA RIADHA. KUTOKA KULIA NI MIHANGWA DEDE KUTOKA LYUSA SEC.

LYUSA Vs MEATU.

TIMU YA LYUSA SEC.
TIMU YA MEATU SEC.

        MICHEZO YA UMISETA ILIYOFANYIKA SIKU YA JUMATATU 11/03/2013.

Wednesday, February 27, 2013

NETIBOLI KIDATO CHA PILI NA KWANZA

Kidato cha Pili (2013)

Kidato cha Kwanza (2013)
Katika mpambano huo kidato cha pili walishinda seti saba kwa moja dhidi ya kidato cha kwanza.

KIKAO

Kikao  kujadili maendeleo ya shule.

MECHI YA MARUDIO KATI YA KIDATO CHA NNE NA CHA PILI



Timu ya kidato cha nne na pili katika picha ya pamoja

Mpambano ukiendelea kwa kasi.
Kidato cha pili wakifunga goli lao la pili. Kidato cha nne walishinda kwa 4-2




Katika mechi hiyo iliyofanyika siku ya jumatano tarehe 27/02/2013 kidato cha nne waliweza kujiondokea na magoli 4 huku kidato cha pili wakifanikiwa kurudisha magoli mawili ya kufutia machozi.

Monday, February 25, 2013

JE TUNAVITUNZA VIPAJI VYA WATOTO?



kijana huyu kwa jina Luhende Castory mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari lyusa ailiyopo katika kijiji cha nkoma wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu, Alikutwa na mpiga picha wetu akimtoa nyoka aina ya Kifutu aliyekuwa ameingia kwenye jengo la choo kinacho tumiwa na wanafunzi kwa kutumia mikono yake bila ya kuzurika. Baada ya mahojiano na kijana huyo, alisema kuwa nyoka  anasumu kali lakini yeye anajua jinsi ya kumzuia asimzuru kutokana mafunzo ya kushika nyoka aliyopatiwa na wataalamu wa jadi. Pia aliongezea kuwa yeye ana uwezo wa kumtibu mtu aliye ng'atwa na nyoka kwa kuvaa shati lake au nguo yake yeyote.



Saturday, February 23, 2013

WALIMU KATIKA POZI.

Walimu wa Lyusa S.S wakiwa katika kibaraza cha nyumba yao kutoka kushoto ni Mwl Manamba C, Theresia Tembo, Kassim Maguluko, Geofrey Mbingamno na Mnzava T, pamoja na Jacob mtoto wa Mwalimu Mashiba.

Friday, February 22, 2013

SIKU YA MICHEZO

Kidato cha Pili (2013)
Kidato cha Nne (2013)
Mechi iliyofanyika siku ya  Ijumaa tarehe 22/02/2013 kati ya kidato cha Pili na Kidato cha Nne. Kidato cha Pili walishinda goli 4-2 zidi ya kidato cha nne ikiwa ni mchakato wa kuunda timu mpya ya shule ambayo itakuwa na wachezaji kutoka katika vidato vya 1 hadi 4.

TUNAHITAJI JENGO LA UTAWALA

Ofisi ya walimu shule ya sekondari lyusa.

TIMU YA NETIBOLI LYUSA

Timu ya netiboli shuleni Lyusa katika picha ya pamoja.

TUNATAKA JENGO LA MAABARA LIKAMILISHWE

Huu ndio msingi wa jengo la maabara ya sayansi katika shule ya sekondari lyusa kama unavyoonekana katika picha msingi huo una miaka zaidi ya minne tokea umeanza kujengwa na haijulikani jengo litakamilika lini. 

JE TUTAFIKA?

Siku hiyo wenyeji waliitwa 1. Takataka 2. Wavuta madawa ya kulevya. KISA?? Wamehoji kuhusu ujenzi wa nyumba mpya ambayo haijaanza kujengwa.

Thursday, February 21, 2013

POPO NI NDEGE AU MNYAMA?

Hawa ni baadhi ya popo wanaoishi kati paa la moja ya nyumba za  walimu shuleni hapa, Popo  wamekuwa wengi kiasi kwamba wanakua kero kwa wakazi wa nyumba hizo, wanasambaza utitiri, vinyesi na mikojo vinatapakaa kila sehemu ndani ya nyumba. Tunaomba kuboreshewa majengo haya ili tuondokane na kero hii.

KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFUNDISHAJI WA MASOMO YA SAYANSI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI TANZANIA

Mtafiti Maganga Musa kutoka Mwambegwa akiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Lyusa wakati alipokuja kukusanya taarifa za ufundishwaji wa masomo ya sayansi katika shule hiyo.

Mtafiti Maganga Musa akiwa katika msingi wa maabara ya sayansi katika shule ya sekondari Lyusa ambao una miaka zaidi ya minne tokea ulipoanza kujengwa. *Jengo lilianza kujengwa mwaka 2008

HIVI KWA MTINDO HUU KUTASOMEKA KWELI?

Kutokuwepo  kwa madaraja katika mito mingi hapa kata ya Nkoma wilaya ya Meatu, kunachangia kuongeza utoro kwa wanafunzi kwani mvua kubwa zinaponyesha mito hiyo hufurika maji mengi kiasi cha kufanya wanafunzi na watu wengine kushindwa kuvuka, hali hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi na wakazi wengine wa kata. Hali hii inarudisha nyuma maendeleo. Pichani mwanafunzi wa shule ya msingi Nkoma akiwa ameshindwa kuvuka mto lyusa baada ya kufurika na maji mengi.