Kutokuwepo kwa madaraja katika mito mingi hapa kata ya Nkoma wilaya ya Meatu, kunachangia kuongeza utoro kwa wanafunzi kwani mvua kubwa zinaponyesha mito hiyo hufurika maji mengi kiasi cha kufanya wanafunzi na watu wengine kushindwa kuvuka, hali hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi na wakazi wengine wa kata. Hali hii inarudisha nyuma maendeleo. Pichani mwanafunzi wa shule ya msingi Nkoma akiwa ameshindwa kuvuka mto lyusa baada ya kufurika na maji mengi. |