Monday, February 25, 2013

JE TUNAVITUNZA VIPAJI VYA WATOTO?



kijana huyu kwa jina Luhende Castory mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari lyusa ailiyopo katika kijiji cha nkoma wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu, Alikutwa na mpiga picha wetu akimtoa nyoka aina ya Kifutu aliyekuwa ameingia kwenye jengo la choo kinacho tumiwa na wanafunzi kwa kutumia mikono yake bila ya kuzurika. Baada ya mahojiano na kijana huyo, alisema kuwa nyoka  anasumu kali lakini yeye anajua jinsi ya kumzuia asimzuru kutokana mafunzo ya kushika nyoka aliyopatiwa na wataalamu wa jadi. Pia aliongezea kuwa yeye ana uwezo wa kumtibu mtu aliye ng'atwa na nyoka kwa kuvaa shati lake au nguo yake yeyote.