Thursday, February 21, 2013

POPO NI NDEGE AU MNYAMA?

Hawa ni baadhi ya popo wanaoishi kati paa la moja ya nyumba za  walimu shuleni hapa, Popo  wamekuwa wengi kiasi kwamba wanakua kero kwa wakazi wa nyumba hizo, wanasambaza utitiri, vinyesi na mikojo vinatapakaa kila sehemu ndani ya nyumba. Tunaomba kuboreshewa majengo haya ili tuondokane na kero hii.