Wednesday, February 27, 2013

NETIBOLI KIDATO CHA PILI NA KWANZA

Kidato cha Pili (2013)

Kidato cha Kwanza (2013)
Katika mpambano huo kidato cha pili walishinda seti saba kwa moja dhidi ya kidato cha kwanza.

KIKAO

Kikao  kujadili maendeleo ya shule.

MECHI YA MARUDIO KATI YA KIDATO CHA NNE NA CHA PILI



Timu ya kidato cha nne na pili katika picha ya pamoja

Mpambano ukiendelea kwa kasi.
Kidato cha pili wakifunga goli lao la pili. Kidato cha nne walishinda kwa 4-2




Katika mechi hiyo iliyofanyika siku ya jumatano tarehe 27/02/2013 kidato cha nne waliweza kujiondokea na magoli 4 huku kidato cha pili wakifanikiwa kurudisha magoli mawili ya kufutia machozi.

Monday, February 25, 2013

JE TUNAVITUNZA VIPAJI VYA WATOTO?



kijana huyu kwa jina Luhende Castory mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari lyusa ailiyopo katika kijiji cha nkoma wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu, Alikutwa na mpiga picha wetu akimtoa nyoka aina ya Kifutu aliyekuwa ameingia kwenye jengo la choo kinacho tumiwa na wanafunzi kwa kutumia mikono yake bila ya kuzurika. Baada ya mahojiano na kijana huyo, alisema kuwa nyoka  anasumu kali lakini yeye anajua jinsi ya kumzuia asimzuru kutokana mafunzo ya kushika nyoka aliyopatiwa na wataalamu wa jadi. Pia aliongezea kuwa yeye ana uwezo wa kumtibu mtu aliye ng'atwa na nyoka kwa kuvaa shati lake au nguo yake yeyote.



Saturday, February 23, 2013

WALIMU KATIKA POZI.

Walimu wa Lyusa S.S wakiwa katika kibaraza cha nyumba yao kutoka kushoto ni Mwl Manamba C, Theresia Tembo, Kassim Maguluko, Geofrey Mbingamno na Mnzava T, pamoja na Jacob mtoto wa Mwalimu Mashiba.

Friday, February 22, 2013

SIKU YA MICHEZO

Kidato cha Pili (2013)
Kidato cha Nne (2013)
Mechi iliyofanyika siku ya  Ijumaa tarehe 22/02/2013 kati ya kidato cha Pili na Kidato cha Nne. Kidato cha Pili walishinda goli 4-2 zidi ya kidato cha nne ikiwa ni mchakato wa kuunda timu mpya ya shule ambayo itakuwa na wachezaji kutoka katika vidato vya 1 hadi 4.

TUNAHITAJI JENGO LA UTAWALA

Ofisi ya walimu shule ya sekondari lyusa.

TIMU YA NETIBOLI LYUSA

Timu ya netiboli shuleni Lyusa katika picha ya pamoja.

TUNATAKA JENGO LA MAABARA LIKAMILISHWE

Huu ndio msingi wa jengo la maabara ya sayansi katika shule ya sekondari lyusa kama unavyoonekana katika picha msingi huo una miaka zaidi ya minne tokea umeanza kujengwa na haijulikani jengo litakamilika lini. 

JE TUTAFIKA?

Siku hiyo wenyeji waliitwa 1. Takataka 2. Wavuta madawa ya kulevya. KISA?? Wamehoji kuhusu ujenzi wa nyumba mpya ambayo haijaanza kujengwa.

Thursday, February 21, 2013

POPO NI NDEGE AU MNYAMA?

Hawa ni baadhi ya popo wanaoishi kati paa la moja ya nyumba za  walimu shuleni hapa, Popo  wamekuwa wengi kiasi kwamba wanakua kero kwa wakazi wa nyumba hizo, wanasambaza utitiri, vinyesi na mikojo vinatapakaa kila sehemu ndani ya nyumba. Tunaomba kuboreshewa majengo haya ili tuondokane na kero hii.

KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFUNDISHAJI WA MASOMO YA SAYANSI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI TANZANIA

Mtafiti Maganga Musa kutoka Mwambegwa akiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Lyusa wakati alipokuja kukusanya taarifa za ufundishwaji wa masomo ya sayansi katika shule hiyo.

Mtafiti Maganga Musa akiwa katika msingi wa maabara ya sayansi katika shule ya sekondari Lyusa ambao una miaka zaidi ya minne tokea ulipoanza kujengwa. *Jengo lilianza kujengwa mwaka 2008

HIVI KWA MTINDO HUU KUTASOMEKA KWELI?

Kutokuwepo  kwa madaraja katika mito mingi hapa kata ya Nkoma wilaya ya Meatu, kunachangia kuongeza utoro kwa wanafunzi kwani mvua kubwa zinaponyesha mito hiyo hufurika maji mengi kiasi cha kufanya wanafunzi na watu wengine kushindwa kuvuka, hali hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi na wakazi wengine wa kata. Hali hii inarudisha nyuma maendeleo. Pichani mwanafunzi wa shule ya msingi Nkoma akiwa ameshindwa kuvuka mto lyusa baada ya kufurika na maji mengi.

Saturday, February 2, 2013

MUONEKANO WA MAZINGIRA NJE YA UZIO WA SHULE!!




NYUMBA MBILI TU!! INAWEZEKANA?


Ndio nyumba zetu pekee ambazo haziwezi kumudu ongezeko la walimu wapya. Hali hii inawalazimisha baadhi ya wafanyakazi kupangisha vyumba katika mji wa mwanhuzi.

TATIZO LA UHABA WA NYUMBA ZA WALIMU

Chumba hiki kidogo kinatumika kama makazi ya walimu wawili shuleni hapa na ikiwa ni kinyume  na matumizi yaliyokusudiwa kwa ajili ya chumba hiki kutumika kama stoo. Hapa ilikuwa siku ya kukifanyia usafi ili majamaa waingie humo.